KATIKA kutekeleza tamko la Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) la
kufika Dodoma kusaidiana na Jeshi la Polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Bavicha Dodoma wameanza maandalizi ya kupokea
vijana zaidi ya 2000.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana Malambaya Manyanya,
Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Dodoma alisema, kwa sasa viongozi wa mkoa
wameanza maadalizi ya kuwapokea wageni wao ambao wanatarajiwa kuanza
kuwasili tarehe 21 na 22 Julai mwaka huu.
Alisema, maadalizi hayo ni ya kuwapokea vijana ambao watatoka katika
mikoa yote ya Tanzania kwa lengo la kutimiza tamko la Bavicha taifa la
kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuzuia mikutano na vikao
vya CCM.
Alisema, kwa sasa mkoa tayari umeunda kikosi cha kufanya kazi ya
maadalizi ya ugeni huo ambapo kwa nia njema utafika mjini Dodoma
kutekeleza kauli ya Rais John Magufuli ya kuzuia vikao vyote na mikutano
ya vyama vya siasa.
Alisema, maadalizi hayo ya kuwapokea vijana hao ni pamoja na viongozi wa
kitaifa wa Bavicha kwa maana ya kutafuta mahali pa kulala na maandalizi
ya chakula.
“Wapo watu ambao wanadhani Bavicha wana mpango wa kufanya fujo, sisi
tunataka kurejesha Demokrasia nchini na kutekeleza kauli ya mkuu wa
nchi.
“Tumekuwa tukiona jinsi mikutano ya Chadema inavyozuiliwa, na sasa
msimamo wa Bavicha ni kuzuia mkutano ya CCM unaotarajiwa kufanyika
Julai 23 kwa lengo la kubadilishana uongozi kati ya mwenyekiti wa sasa
wa CCM na rais msitaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete na Rais John
Magufuli.
“Tumeandaa vijana takribani 2000 kutoka mikoa yote nchini watakaokuja
Dodoma kusaidiana na Jeshi la Polisi kutawanya mkutano usio halali wa
CCM.
“Kwa sababau mkuu wa nchi ametoa tamko la kuzuia mikutano yote ya siasa
ikiwa ni pamoja na vikao vya ndani na mikutano ya hadhara hadi 2020.”
Alisema Malambaya.
Alisema, Jeshi la Polisi lilizuia mikutano ya vyama vya siasa vya
upinzani na mahafali ya Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Chadema
(CHASO) na kuwa, sasa wanashirikiana na polisi kuhakikisha mikutano ya
CCM haitafanyika.
Chadema: Maandalizi ya Kuuzuia Mkutano wa CCM Yameanza
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website