Home » » MCHUMBA WA MTU AAGA ANAKWENDA KWA BIBI YAKE MGONJWA KUMBE ANAENDA KUUZA MWILI WAKE..AKAMATWA

MCHUMBA WA MTU AAGA ANAKWENDA KWA BIBI YAKE MGONJWA KUMBE ANAENDA KUUZA MWILI WAKE..AKAMATWA

Stori: Issa Mnally na Dustan Shekidele, Morogoro
OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers si mchezo! Safari hii imenasa tukio la mchumba wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Jose kuuza mwili.

Tukio hilo lilijiri eneo maarufu la Baa ya Kaumba iliyopo katikati ya mji kwenye Mtaa wa Makongoro, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo OFM na polisi walikuwa kwenye oparesheni za kufichua uovu wa biashara haramu ya ngono.

Kwa mujibu wa mchumba huyo katika mahojiano na OFM, aliaga kwao Kilosa kuwa anakwenda Morogoro mjini kumuuguza bibi yake ambaye ni mgonjwa.

OFM NOMA: Mchumba wa mtu na wenzake wakiwa mikononi mwa OFM na Polisi.
Tofauti na matarajio ya familia yake, mrembo huyo alikwenda kukita kambi maeneo hayo akijihusisha na biashara hiyo haramu eti kwa madai ya kusaka fedha ya kununulia sare za harusi yake ambayo inatarajiwa kufanyika Februari 15, mwaka huu.

Jumatano iliyopita, OFM ilipokea simu kutoka kwa dada mmoja ambaye alieleza kuwa kuna ‘shori’ ambaye ni mchumba wa mtu anajiuza katika viunga vya Kaumba.

Dada huyo aliendelea kueleza kuwa yeye ni mmoja wa wajumbe katika kikao cha harusi ya dada huyo huku akiwa ameshachangia shilingi elfu 50 lakini alishangaa kumuona maeneo hayo hatarishi.

“Niamini mimi, tunakaa naye Mji Mpya (Morogoro). Hata fedha za advance ya ukumbi, vinywaji, MC na muziki tumeshalipa na harusi yake inatarajiwa kufanyika Februari 15, mwaka huu.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, kikosi kazi cha OFM kiliingia mzigoni kwa kushirikiana na dada huyo ambaye alivalishwa ‘beji’ yao na kufanikisha kunaswa kwa mchumba huyo.

OFM ikishirikiana na polisi wanaojua kujituma kwenye majukumu yao walimtia mbaroni dada huyo akiwa katika pilikapilika zake za kunasa wanaume huku mmoja wa vijana wa OFM akijifanya mteja na kupatana naye bei ya kuingia chumbani kwa ‘shoti taimu’.

Baada ya kunaswa, mwanadada huyo alikiri mbele ya OFM kuwa ni bibi harusi mtarajiwa.
“Jamani… jamani ni kweli mimi ni mchumba wa mtu, shetani ameniponza nisameheni,” alisema.

Hata hivyo, kilio chake kiligeuka cha samaki kwani hakikusikika, yeye na wenzake walionaswa walipelekwa moja kwa moja katika kituo kikuu cha polisi ili kupisha sheria ichukue mkondo wake.
---gpl--
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
 
Copyright © 2011. PERUZI HABARI - All Rights Reserved
Proudly powered by Peruzitz