Kwenye zile stori za kwenye mitandao ambazo zimefatiliwa sana ni pamoja
na hii ya Ommy Dimpoz kukutana na Wayne Rooney mchezaji wa Manchester
United wakiwa Ibiza na kisha kupiga picha ambayo imebeba vitu vingi
tusivyovifahamu na pengine tulihitaji kufahamu.
Picha ambayo imepigwa na Dimpoz ni picha ya video ambayo wanaonekana
wanazungumza kitu lakini sauti ya video hiyo imezimwa (mute) so wakati
tunasubiri Ommy Dimpoz mwenyewe atuambie walichokuwa wanazungumza ninayo
hiyo video mtu wangu ambayo Ommy Dimpoz kapost kwenye akaunti yake ya
Instagram.
Kwenye post zake Ommy Dimpoz ameonekana akila raha sehemu mbalimbali za
Ibiza,mahali ambako mastaa wengi wa Dunian hutembelea kwa ajili ya
mapumziko.
Ommy Dimpoz na Wayne Rooney Kwenye Selfie ya Pamoja…
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website