Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh, Mwigulu Nchemba(kulia), na Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto) wakimsikiliza
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, muda mfupi baada ya
Rais Dkt. John Magufuli kumwapisha Waziri Mwigulu Nchemba kuongoza
wizara hiyo leo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Nchemba(Kushoto), akikaribishwa
Makao Makao ya Wizara hiyo na Katibu Mkuu Meja Jenerali Projest
Rwegasira.Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamad Masauni
na wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Yahya Simba.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akisalimiana na Mkuu wa
Kitengo cha Teknolojia ya Mawasiliano, Jane Massawe, mara baada ya
kupokelewa Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiweka saini mara baada ya
kuwasili Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi muda mfupi
baada ya kuapishwa kwake. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja
Jenerali Projest Rwegasira na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Yahya
Simba.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)