Hii ni habari ya motomoto kabisa! Mama la mama, Zarinah Hassan ‘Zari The
Boss Lady’ amedaiwa kunasa ujauzito wa mpenzi wake, Mbongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Risasi Mchanganyiko lina ubuyu
ulionyooka.
Taarifa hizo za ndani ya familia zimevuja ikiwa ni takriban miezi nane
tangu mrembo huyo ampe jeuri Diamond ya kutembea kifua mbele kwa
kumzalia Tiffah ambapo inaelezwa kuwa, amefanya hivyo makusudi kuwakata
‘vilimilimi wabaya’ wake.Zarimond
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kutoka ndani ya familia ya Wasafi Classic Baby (WCB),
juzikati kilinyetisha kuwa, gumzo la mjini kwa sasa ni wadau wa burudani
kujadili ujauzito wa Zari, ambao unaonekana kuwatisha karibia wapambe
wote wa timu pinzani.
“Naomba nikudokeze juu ya Zari kuwa mjamzito tena, habari hii ni ya
uhakika na kila mtu WCB anajua, Zari amenyaka mimba na cha ajabu
amekataa katakata kuichomoa kama Diamond alivyokuwa akimshawishi.
NDIYO CHANZO CHA UGOMVI
“Huwezi kuamini ugomvi wote ambao umekuwa ukidaiwa kuendelea kati ya
Diamond na Zari umesababishwa na ujauzito huo ambapo Diamond amekuwa
akitumia nguvu nyingi kumuomba Zari achomoe mimba hiyo lakini hakuna
hata siku moja ambayo ameonesha dalili za kumuelewa.
MIMBA INA MIEZI MINNE
Chanzo hicho kilizidi kuweka bayana kuwa, kinachomsikitisha Diamond ni
kwamba, mimba hiyo inazidi kukua jambo ambalo anaona si sahihi kwa sasa
kwani ana mtoto (Tiffah) ambaye bado hajatimiza hata mwaka mmoja.
“Jamaa anaona soo, anaona kama jamii haitamuelewa hivi, jitihada zake za
kumshawishi zinagonga ukuta na mbaya zaidi mimba kwa sasa ina kitu kama
miezi minne,” kilisema chanzo hicho makini.
SAFARI ZA SAUZ ZATAJWA
Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, safari ambazo Diamond alikuwa
akizifanya mara kwa mara kwenda Afrika Kusini (Sauz), nyingi zilikuwa
ni za kutatua mgogoro huo ambao umeikumba familia ya WCB, kiasi kwamba
hadi wazazi wote wameshirikishwa lakini mwisho wa siku hakuna muafaka.
“Si unakumbuka kuna kipindi Diamond alikuwa anakwenda Sauz mara kwa
mara, ishu hiyo ndiyo ilikuwa inampeleka lakini hazikuzaa matunda, mamaa
kagoma,” kilisema chanzo hicho.
FAMILIA YAKE YAMSHANGAA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, familia yake imemshangaa
Diamond kwa nini hakuwa makini wakati alijua kabisa Tiffah bado angali
mdogo.
“Wamemshangaa sana kwa kushindwa kuwa makini wakati kwa sasa kuna mbinu
nyingi sana za kuepuka ujauzito, sasa matokeo yake amesababisha hadi
kuwe na mvutano unaokosa muafaka,” kilisema chanzo hicho.
NDUGU WA DIAMOND ATHIBITISHA
Mwanahabari wetu alipokuwa akiichimba habari hii, alizungumza na mmoja
wa ndugu wa Diamond ambaye alikiri kuwa Zari ni mjamzito lakini akaombwa
asitajwe jina maana suala hilo limegubikwa na usiri mzito.
“Ndiyo hivyo kama ulivyosikia. Zari hataki kutoa, nahisi kwa sababu ya
kuwakomesha zile timu pinzani lakini anashindwa kujua upande wa pili
familia inashindwa kukubaliana naye maana ni jambo la aibu kupata mimba
kabla mtoto wa awali hajafikisha hata mwaka,” alisema ndugu huyo.
MSIKIE DIAMOND
Baada ya kupenyezewa ubuyu huo wa motomoto, Risasi Mchanganyiko
lilimtafuta Diamond mwenyewe ili aweze kuweka bayana habari hiyo ya
heri, ambapo hakutaka kukataa wala kukubali licha ya kukiri kuzisikia
habari hizo.
“Dah! Habari hizi sijui muda mwingine huwa mnazinyaka vipi, sijui hapa
niseme nini zaidi ila unachotakiwa kufahamu mimi bado nahitaji kupata
watoto zaidi ya mmoja na ifahamike kuwa ninapenda watoto sana, maana
uwezo wa kuwahudumia ninao hata hivyo kushika mimba kwa Zari ni mapema
sana,” alisema Diamond.
MAMA YAKE NAYE
Mama mzazi wa msanii huyo, Sanura alitafutwa ili kusikia maoni yake,
lakini badala yake, aliishia kucheka na kumuomba mwandishi wa habari
hizi kuachana na mambo hayo.
Chanzo:Global Publishers
Zari Anasa Ujauzito Tena!
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website