Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni ametangaza vita dhidi ya majambazi na watu wanaojihusha na mauaji.
Alisema Serikali imelazimika kutangaza vita hivyo baada ya kutokea
matukio 41 yaliyohusisha mauaji ya kinyama tangu Januari hadi mwezi
uliopita.
“Serikali ipo kazini, sasa inatangaza vita dhidi ya watu wanaojihusisha
na ujambazi, watakaobainika hakika wataangamizwa hatuwezi kukubali watu
wazidi kupoteza maisha pasipo na sababu za msingi,” alisema Masauni.
Waziri huyo alitembelea Msikiti wa Rahman Mtaa wa Utemini Kata ya
Mkolani wilayani Nyamagana, Mwanza na kusema matukio hayo yanapaswa
kutokomezwa na kukemewa kwa nguvu zote.
“Mauaji hayo yalikuwa ya kutisha hivyo ilikuwa ni lazima watuhumiwa
wakamatwe, hata hao waliokimbia wanapaswa kutiwa mbaroni,” alisema.
Pia, alionya tabia ya baadhi ya polisi kujihusha na vitendo vya uhalifu na kupoteza imani na uaminifu kwa wananchi.
Aliwataka polisi wanaofanya vitendo hivyo kuacha na badala yake wapambane na wahalifu.
Masauni alisema nia ya Serikali ni kuhakikisha Watanzania wanaishi kwa
utulivu, hivyo haitakubali watu wachache kuvuruga amani iliyopo
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema vyombo vya usalama vipo
imara kwani baadhi ya wahalifu wameuawa na wengine kukamatwa na
wanaendelea kuhojiwa.
Mjumbe wa baraza la masheikh Wilaya ya Nyamagana, Saidi Darwesh alisema
tukio la mauaji ya msikitini limesababisha hofu kwa waumini, hususan
kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani kwani wengine hawaendi msikitini
kuswali.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Utemini, Jukael Kiula alisema wakazi
wa Kata ya Mkolani wamejitolea kujenga kituo cha polisi katika mtaa huo
ili kudhibiti uhalifu unaotokea mara kwa mara
Home »
KITAIFA
,
SIASA
» Serikali Yatangaza Vita Dhidi ya Majambazi na Watu Wanaojihusisha na Mauaji
Serikali Yatangaza Vita Dhidi ya Majambazi na Watu Wanaojihusisha na Mauaji
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website