Polisi mkoani Kahama wametumia mabomu ya machozi kutawanya makundi ya
wananchi wanaokutwa wamekusanyika katika maeneo mbalimbali.
Mabomu hayo yameendelea kurindima katika viwanja vya CDT ili kuwatawanya
wananchi hao waliokusanyika kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa hadhara
wa Chadema.
Mkutano huo ulipangwa kufanyika leo kuanzia saa 9.00 alasiri kabla ya
polisi kuupiga marufuku na jeshi hilo kuzuia mikutano mingine kama hiyo
nchini.
Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jioni la leo na
Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Nsato Mssanzya amepiga
marufuku maandamano na mikutano ya hadharahadi hali ya usalama
itakapotengemaa.
Amesema Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu yoyote au chama chochote kitakachokaidi agizo hilo.
Polisi Watumia Mabomu ya Machozi Kuwatawanya Wafuasi wa CHADEMA
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website