Leo
June 08 2016 Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefika Makao makuu
kanda maalum ya Dar es salaam, ikiwa ameitikia wito wa polisi. Zitto
amefika kituoni hapo na ametakiwa atoe maelezo kuhusiana na maudhui ya
hotuba ambayo aliitoa June 5 2016.
Kupitia
ukurasa wake wa facebook chama cha ACT Wazalendo kimeainisha masuala
matano muhimu yaliyoibuka wakati wa mahojiano ya Kiongozi wa Chama Cha
ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na Polisi, Leo Jijini Dar es salaam.
1.Maombi ya Chama Cha ACT Wazalendo ya mkutano ilikuwa ‘Kujenga Chama’ Lakini Chama Kilizindua “Operesheni Linda Demokrasia”.
2. Kusema “Rais Ameropoka kuhusu Sakata la Sukari Nchini”
3. Kumchonganisha Rais na Wananchi kuhusu suala la kuwaita Vijana wa Kitanzania Kuwa ni “Vilaza”
4.
Kumgombanisha Rais na Wananchi kwa Kusema “Yeye anajifanya Rais wa
Masikini (Huku akiwakashifu hao Watoto wa Masikini Kwa Kuwaita “Vilaza”)
na hivyo kumgombanisha na wasio Masikini”
5. Kumwita Rais Dikteta na Kwamba anaendesha Nchi Kiimla
Kupitia
ukurasa huo wametoa taarifa kuwa maelezo ya Jeshi la Polisi ni Kuwa
yote hayo yanaangukia kwenye Kifungu Cha 89(1)(a) cha Penal Code, Yaani
“Kutumia Maneno ya Matusi yenye Kuweza Kuvunja Amani” (Abusive
Language).
Jeshi
la Polisi limemuomba Zitto afike Tena Kituoni Hapo Juni 15, 2016
Kwaajili ya Mahojiano zaidi. Mwanasheria wa Ndugu Zitto ameliomba Jeshi
la Polisi kupeleka Mashtaka Mahakamani Juu ya Suala Husika, Na Kwamba
Ndugu Zitto atakwenda Kuthibitisha Ukweli Na Undani wa Masuala hayo
Mahakamani
Mambo Matano Yaliyoibuka Wakati wa Mahojiano ya Zitto Kabwe na Polisi
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website