Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa Wa Arusha,imemhukumu Isack Habakuki(40)
mkazi Wa Olasiti, kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya
shilingi milioni 7 kwa kosa la kumtukana Rais Magufuli kupitia mtandao
wa facebook.
Mshtakiwa amekiri kutenda kosa hilo na amekubali kulipa faini ambapo
mahakama imeamuru alipe fedha hizo kwa awamu mbili. Katika awamu ya
kwanza atalipa July 8 2016 sh mil 3.5 na August 8 2016 atalipa kiasi
kilichobaki cha sh mil 3.5.
Isack anayeishi Kata ya Olasite, anadaiwa kutoa lugha ya matusi na
dhihaka kwa Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook na
alikamatwa Machi 23, mwaka huu mjini Arusha na kupelekwa Makao Makuu ya
Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam kisha alirejeshwa tena Arusha
Aprili 14, mwaka huu kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka.
Mbele ya Hakimu Mkazi, Augustine Rwizile, Wakili wa Serikali, Gaudensia
Massanja, alidai kuwa Isack alikuwa akikabiliwa na kosa moja ambapo kwa
kufahamu na kwa makusudi mtuhumiwa huyo alitumia mtandao wa Facebook
kwa nia ya kumtukana Magufuli.
Alidai kwamba mtuhumiwa katika ukurasa wake wa Facebook alichangia
maneno yanayosema: “Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha huyu
bwege na Nyerere wapi buana.”
Home »
KITAIFA
,
SIASA
» Aliyemtukana Rais Magufuli , Isaac Emily Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 3 Jela au Kulipa Faini Ya Sh. Milioni 7
Aliyemtukana Rais Magufuli , Isaac Emily Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 3 Jela au Kulipa Faini Ya Sh. Milioni 7
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website