Hakikisha unawakwepa aina hii ya wanawake ili usijiingize kwenye matatizo. Nitakwambia ni kwa nini…..
1.Demu wako wa zamani
Ni vizuri kutorudia mahusiano ya zamani
na zaidi kama kwenye mahusiano yenu ya mwanzo mambo hayakuishia kwa
uzuri. Sababu kuu ya msingi, kiukweli ni kwamba hakika mwanzoni mlikuwa
hamuendani na ndio sababu ya iliyopelekea kuvunjika kwa mahusiano yenu,
ndani ya hizo sababu kuna vitu vilivyopolekea kutokea kwa hayo,
ukichunguza na kuziangalia kwa makini utagundua ni za asili na ambazo si
rahisi kwa mmoja wenu kuzibadilisha sababu ni vitu au mambo ambayo
yatakuwa ni ya damuni.
2.Dada wa rafiki yako kipenzi
Epukana na kujiingiza kwenye mahusiano
na dada wa rafiki yako. Si tu kwamba utaweza kujiingiza kwenye uhasama
na chuki kama mambo hayatakwenda sawa, ila pia utaweza kujiweka kwenye
mazingira ya kujikuta siku moja unapigwa hata ngumi za uso sababu tu
ulimuumiza dada yake. Pia, utaweza kumkosa mtu ambaye ndie alikuwa ni
kimbilio lako kwa mambo mbalimbali pale ambapo itatokea wewe na dada
yake mambo kutokwenda sawa, sababu hapo patakuwa na mgongano wa
kimaslahi kwa huyo rafiki yako.
3.Wanawake wenye mambo mengi
Kiukweli, kutoka na watu kama hawa
kinaweza kuwa ni kitu cha kufurahisha, ila mwisho wa siku itakuingiza
kwenye matatizo. Mara zote kumbuka ni vyema kuwa salama kuliko kujuta.
Usijiingize kwenye majaribu ambayo utakuja kuyajutia kwa maisha yako
yote.
4.Wanawake wanaopenda hela kupitiliza (Wachunaji)
Kuwa mbali nao, labda kama unataka salio
lako limalizike pasipo wewe kujifahamu. Naamini hili kila mmoja
analifahamu na halihitaji darasa zaidi.
5.Demu wa zamani wa rafiki yako
Kama unathamini urafiki wako na mshikaji
wako achana na habari ya kutoka na aliyekuwa demu wake. Mambo yanaweza
kubadilika na kuwa kama au zaidi ya yaliyotokea kwa rafiki yako na ikaja
kula kwako zaidi. Wakati mwengine inaweza tengeneza chuki kati yako na
rafiki yako, huku akiamini kwamba ulikuwa unatoka au kumnyemelea demu
wake toka zamani.
Wadau mademu wapo wengi sana, fanya kutafuta wengine nje ya hawa….. ni ushauri tu
JE, UNAJUA AINA YA WANAWAKE HATARI KUWA NAO ..
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website