KIMENUKA! Mwigizaji Jacqueline Wolper ameibua tafrani la aina yake kwa
Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ baada ya kumtumia
meseji iliyomtia shaka mpenzi wa staa huyo, Siwema.
Tukio hilo lilitokea juzikati nyumbani kwa Nay wa Mitego, Kimara-
Korogwe jijini Dar ambapo ilisemekana Wolper alituma SMS iliyokuwa
ikiuliza muafaka wa jambo fulani ndipo Siwema akaja juu na kuanza
kumcharukia bebi wake huyo.
Alipoulizwa Nay wa Mitego kuhusiana na ugomvi huo, alifunguka:
“Wolper ni rafiki yangu kitambo, ni mtu wangu tunayeelewana kupita
maelezo, hivyo juzikati nilikuwa nikichati naye juu ya kutaka
kumshirikisha kwenye video ya wimbo wangu mpya wa Akadumba, Siwema
dizaini kama alimaindi kuona nawasiliana naye lakini nilimuelewesha na
kila kitu kipo sawa.”
JACK WOLPER NUSURA ATIBUE UCHUMBA WA ''NAY'' NA ''SIWEMA''
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website