RAIS wa Rwanda, Paul Kagame amenusurika
kifo baada ya msafara wake nchini Kenya kupata ajali na kusababisha watu
wawili kujeruhiwa vibaya. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika
la Habari la Uingereza (BBC), imeelezwa kuwa ajali hiyo ilihusisha
mojawapo ya magari ya msafara wake nchini Kenya, alipokuwa kwenye ziara
za kikazi.
Hata hivyo, Rais Kagame hakujeruhiwa
katika ajali hiyo iliyotokea saa mbili asubuhi jana eneo la Limuru
nchini Kenya. Dereva wa gari hilo alipoteza mwelekeo katika barabara kuu
ya Nairobi-Limuru, hata hivyo gari hilo lilikuwa mbali na msafara wa
rais huyo. Aidha majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa haraka hospitalini.
Rais Kagame alikuwa anarejea mjini Nairobi kutoka katika kongamano la Magavana wa Kenya mjini Naivasha katika Bonde la Ufa.
Kagame alialikwa kuhudhuria kongamano la Magavana nchini Kenya, kuhusu uongozi mzuri na utawala bora
KAGAME ANUSURIKA KIFO NCHINI KENYA
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website