Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amewataka
Watanzania kujali makundi ya watu wenye mahitaji maalumu hususan katika
kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Kauli hiyo aliitoa jana alipotembelea vituo vya watoto yatima jijini
Dar es Salaam vinavyoendeshwa na Waislamu kwa lengo la kuwajenga watoto
kiimani. Lengo la ziara yake ni kushiriki nao katika utekelezaji wa
nguzo ya mfungo wa Ramadhan.
Katika ziara hiyo, Lowassa aliyekuwa ameongozana na waumini mbalimbali
wa dini hiyo, alitembelea vituo vitatu vya yatima ambavyo ni Chakuwama
kilichopo Sinza, Khairat cha Kigogo na Umra kilichopo Magomeni
Mwembechai.
Katika ziara hiyo, Lowassa alitoa msaada wa unga, mchele, mafuta ya kupikia, tende na sukari.
Lowassa alitoa rai kwa watu wenye uwezo kujiweka karibu na jamii
inayohitaji msaada, ili kuenzi utamaduni wa Watanzania kusaidiana.
“Jamii lazima tuangalie makundi haya kwa kushiriki nao pamoja kwenye
mahitaji yao, kula nao pamoja,”alisema.
Mratibu wa misaada hiyo, Sheikh Rajab Katimba ambaye ni Msemaji wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, alisikitishwa na baadhi ya
Waislamu wanaofuturisha makundi ya watu wenye uwezo na kusahau makundi
ya wasiojiweza.
“Tusaidiane Waislamu na inashangaza sana kuona jamii inayohitaji msaada
inasahaulika na kufuturisha wenye kujiweza kiuchumi, siyo mbaya ila
tukumbuke jamii hii yenye uhitaji,” alisema Sheikh Katimba.
Mbali na salamu hizo, dua zilisomwa na watoto wawili, Fadhia Liziki (3) na Nasra Ramadhan (3) wa kituo cha Kigogo kuombea amani.
Asnat Ali (6) wa kituo hicho alitoa shukrani zake, huku akihitaji
ukarimu huo uguse kundi la Watanzania wengine walio na nafasi ya
kiuchumi. Saida Hassan ambaye ni mmiliki wa kituo cha Sinza chenye
watoto 90, alishukuru misaada hiyo huku akiomba ushirikiano zaidi wa
kulea watoto hao.
“Kwa upande wetu tunashukuru na tunamwombea aendelee kuwa na moyo huo wa
utoaji, msaada huu utatusaidia sana kwenye mwezi huu mtukufu,” alisema
Rahima Juma Kishunda ambaye ni mmiliki wa kituo cha yatima Umra
Lowassa Asaidia Watoto Yatima Dar es Salaam
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website