Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mwigulu
Nchemba, ambaye jana alikuwa miongozi mwa manaibu waziri walioapishwa
na Rais Jakaya Kikwete kushika nyadhifa zao amewaambia watu wanaoponda
uteuzi wake kuwa hana haja ya kubishana nao kwani hawamjui.
Katika maelezo yake, Mwigulu alisema
anamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kumwamini kuwa anaweza kumsaidia katika
kusimamaia sera na mipango ya fedha nchini. Watu wasionifahamu wanadai
mimi sina viwango vya kufanya kazi hii; naomba wafahamu kuwa mimi ni
msomi mwenye shahada ya ya pili ya uchumi na hivi sasa niko katika
masomo ya kupata shahada ya uzamivu.
Mwigulu aliendelea kusema “Kabla
sijaingia kwenye siasa nilikuwa nafanya kazi katika Benki Kuu ya
Tanzania kama mchumi. Ninakwenda Wizara ya Fedha kusimamia mambo manne
ambayo ni uadilifu, ushirikiano, jitihada na huduma madhubuti ambazo
zitatolewa kwa wakati mwafaka.
Home »
SIASA
» HAYA NDIYO MAJIBU YA MWIGULU NCHEMBA KWENDA KWA WANAOPONDA UTEUZI WAKE,AWEKA WAZI ELIMU YAKE
HAYA NDIYO MAJIBU YA MWIGULU NCHEMBA KWENDA KWA WANAOPONDA UTEUZI WAKE,AWEKA WAZI ELIMU YAKE
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
