Stori: Shani Ramadhani na Mayasa Mariwata
STAA wa wimbo wa Majanga, Snura Mushi
ameingia kwenye majanga baada ya kudaiwa kukacha na deni la prodyuza
Mohammed Kandoro wa Studio za Fire Music ambaye alimrekodia nyimbo
kadhaa wakati akisaka kutoka.
Habari kutoka kwa chanzo cha kuaminika
zinasema kuwa Snura ameingia mitini na kiasi cha Tsh. 400,000 za
prodyuza huyo na kwamba sasa amehamia studio nyingine.
Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya
Kandoro na kumwuliza kuhusu ukweli wa minong’ono hiyo, ambapo alikiri na
kusema: “Ni kweli namdai laki nne. Nimefanya naye kazi kwa muda mrefu
lakini sasa naona ameamua kuondoka na deni langu.”
Snura alipopigiwa simu na kuelezwa
kuhusu madai hayo, alifunguka: “Kama kuna deni basi meneja wangu HK
(Hyper Man) ndiye anayehusika, maana kila kitu nilimkabidhi yeye na
naamini alilipa, sasa kama hakulipa hayo ni mambo yanayomhusu yeye, si
mimi tena.”
Katika kutafuta mzani wa habari, gazeti
hili liliwasiliana na meneja wa Snura, HK ambaye alisema hana deni
lolote analodaiwa na Kandoro, ingawa alikiri kumhamisha Snura studio.
“Kilichopo ni kwamba tumehama kwenye
hiyo studio, sina ugomvi nao wala Snura hajawahi kutofautiana naye.
Tumefanya hivi kwa lengo la kutafuta ladha tofauti... hayo mambo ya
madeni, si kweli.
Hivi kama leo hii tunaweza kulipa zaidi
ya shilingi milioni moja na laki nne (1,400,000) tunashindwaje kulipa
laki nne tu? Hayo ni maajabu,” alisema HK.
Source:GPL
SNURA TUHUMA NZITO...ADAIWA KULIKIMBIA DENI LA PRODUCER WAKE ALIYE MTOA
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
