Lowassa kupitia ukurasa wake wa Facebook ameelezea furaha yake namna
ambavyo ameimarika zaidi baada ya kujitoa ndani ya CCM hadi sasa ambapo
ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.
''Nina furaha kutimiza mwaka mmoja toka nilipojitoa CCM na kujiunga na
CHADEMA.Uamuzi ule haukuwa rahisi,lakini kwa ushupavu, ujasiri na
mwongozo wa Mungu nilifanya hivyo. Nilifanya uamuzi wa kihistoria katika
nchi yetu'' Amesema Lowassa.
Ameongeza kuwa watanzania bado wanataka mabadiliko na hali hiyo imezidi
kuthibitika kuwa wananchi hawawezi kuyapata ndani ya CCM .
Amesema watanzania wanataka sera na mtu mbadala wa kuongoza mabadiliko
hayo na kwamba vyote hivyo watavipata ndani ya CHADEMA na UKAWA kwa
jumla.
Aidha amewataka watanzania wanaomuunga mkono na ambao walihama CCM kwa
ajili yake waendelee kumuunga mkono na kuiunga mkono CHADEMA
Nina Furaha Toka Nitoke CCM - Edward Lowassa
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website