Wanamuziki, Vanessa Mdee na mpenzi wake Juma Jux ‘Jux’ baada ya
manenomaneno kuzagaa kuwa wameachana juzikati wapenzi hao walionekana
kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti iliyopo mkoani Mara kisha kwenda
kula bata kwenye hoteli ya bei mbaya ya Singita.
Akipiga stori na safu hii juzi akiwa Serengeti, Vanessa alisema kuwa,
wameamua kwenda huko kwa mapumziko ya siku nne ikiwa ni sehemu ya
kufanya utalii wa ndani na wamekula bata za kutosha.
“Ni mambo ya utalii wa ndani, tumekuja huku kupumzika kidogo, siyo
lazima kwenda nchi za nje kwa mapumziko, humuhumu Bongo kuna sehemu
unakwenda na unajisikia furaha,” alisema mwanadada huyo.
Singita ni hoteli ya kifahari iliyopo mkoani Mara ambayo inaiingizia nchi fedha nyingi za kigeni
Vanessa Mdee Afungukia Bata Walizokula Singita Hoteli....
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website