Floyd Mayweather amemdunda Manny Pacquiao kwa points baada ya pambano la
dunia lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kumalizika huko jijini Las
Vegas.
Pacquiao kama ilivyokuwa ikitarajiwa alirusha ngumi nyingi zaidi kuliko
mpinzani wake lakini Mayweather aliweza kurusha ngumu zenye faida zaidi
zilizowafanya majaji wanne wampe ushindi.
Mayweather ameshinda kwa point 118-110, 116-112, 116-112. Kwa ushindi
huo, Mayweather ameendelea kushikiliza rekodi yake ya kutowahi kushindwa
katika mapambano yake 48 aliyowahi kupigana.
Tazama picha za pambano hilo.