Kuna matumaini kwa Haji Manara atarejea na kuona kama kawaida baada ya matibabu yake jijini New Delhi nchini India.
Manara amezungumza leo na kusema tayari ameanza vipimo na ana matumaini.
"Nimemaliza vpimo vya awali na kuonyesha matumaini ya kupona. Tayari nishaanza tiba na kesho natarajiwa kulazwa hospitali kwa siku tatu kwa uchunguzi zaid na matibabu.
"Imani imekuwa kubwa kwa majibu ya leo, ambayo yanaonyesha kuvilia na kuganda kwa damu katika macho yangu.
"Madaktari wanasema upo uwezekano mkubwa wa kupona ila watajua zaidi baada ya kumaliza tiba ya awali na uchunguzi," alisema Manara.
Manara amesafirishwa kwenda India baada ya kuamka asubuhi jicho lake likiwa halioni kabisa huku moja likiwa limepoteza uwezo na kubaki kwa asilimia 10 tu.