MBOWE: Ameomba pole kwa kuwashtukiza wanahabari kwa kuwapa taarifa ya ghafla, amemualika Sumaye azungumze na waandishi wa habari pia na watanzania wote, atakaefunga atakua mwenyekiti wa NCCR mageuzi, Sumaye atakuwa na jambo la kulieleza taifa, ni mtu mwenye uwezo mkubwa na anamkaribisha aje kuzumngumza na wanahabari.
Sumaye: Mheshimiwa Lowassa, viongozi, wenyeviti wa UKAWA, ndugu zangu viongozi mbalimbali wanaounda UKAWA. Nimewaita hapa juu ya mambo mawili makubwa.
Moja ni kutoa ufafanuzi kwa jambo lililotokea hivi karibuni kama wiki moja hivi, kuna taarifa zilitoka katika mitandao ya kijamii kadri ya wiki moja iliyopita kuwa nimejitoa CCM na kuhamia UKAWA. Ile taarifa ilikuwa uongo.
Basi kulikuwa na ndugu yangu, ndugu yangu kabisa anayeitwa John Mrema, alipoiona akanipigia simu wakati nipo nje ya nchi kwamba kuna taarifa umejitoa CCM nikamwambia hapana, akasema basi naomba uikanushe, nikamuomba aikanushe kwa niaba yangu ila kwa bahati mbaya naamini kwa nia njema ili kutia msisitizo alienda mbele zaidi na kusema Sumaye hatajitoa CCM maisha yake yote, hiyo si sahihi, hakuna mtu anaweza akafunga nadhiri na chama cha siasa.
La pili akasema Sumaye atazunguka nchi nzima na Magufuli kumnadi, hili nalo si sahihi na bahati nzuri CCM wameshamjibu kwa kutoa orodha ya watu wataomnadi mgombea wa CCM. Napenda kumshukuru ndugu Lema kukanusha taarifahii hata kama aliongezea chumvi za hapa na pale.
Kwanza niseme wazi sina tatizo na mgembea wa CCM ndugu Magufuli na nina raha moyoni yeye ndie mgombea kupitia CCM, ninaamini hakuhonga, mtu anae chapa kazi japo ana mapungufu yake mengi, hakuna mwanadamu aliekamilika.
Mimi nina tatizo na mfumo wetu au mfumo wao katika uchaguzi, kwa sababu kile chama cha mapinduzi ni cha zamani. Mimi kwa imani yangu na naamini imani ya wengi safari hii yametokea sana katika chama cha CCM. Ni vizuri tuige kwa wenzetu waliokomaa kidemokrasia.
Binafsi nilitarajia sitafika mbali katika mchakato huo. Tatizo la rushwa katika CCM, hili linathibitishwa na pesa nyingi zilizotumika wakati wa mchakato, watu waliwanunua wapiga kura.
CCM haikufanya tathmini, kama mgombea urais anadondoka karibu asilimia 20, chama kilitakiwa kishtuke lakini CCM haikustuka, CCM haikuhamasisha uandikishaji na upigaji wa kura. Walizunguka nchi nzima lakini walikuwa hawahamasishi bali wanaivua nguo serikali yao. Umeiweka wewe pia ni kazi yako kuirekebisha wewe. Sura ya utawala katika vyama vingi, lengo ni ili siasa itoe ushindani, lazima ujunge sifa mbili muhimu. Moja mgawanyo wa dhahiri kati ya siasa na utumishi wa umma, kama mgawanyiko huu upo vizuri wanasiasa wanaweza kubadilishwa hata baada ya miezi sita. Katika nchi yetu, mgawanyo huu si dhahiri, inabomoa misingi ya utumishi, jamii hata watu binafsi. Huwa tunasikia nchi kama Italy na nyinginezo waziri mkuu na serikali imeanguka lakini huwezi kusikia athari.
Vyama vingi pia lazima Ijenge sura ya kuwa na vyama viwili vikubwa vinavyolinganangana, hata marekani wana vyama viwili vikubwa, pia Uingereza. Usipokuwa na chama mbadala, ipo siku wananchi wataingiza chama ambacho hakipo tayari madarakani. Hakuna chama cha siasa kinachokaa milele hata kifanye vizuri namna gani, watu watakichoka tu.
Niligombea urais kupitia CCM kutaka kuleta mabadiliko hayo mawili, katika marekebisho hayo, nafasi ya wakuu wa wilaya ningeitoa katika siasa. Ningejenga chama mbadala ndani ya CCM, kwa sababu nilijua kufanya nje ya CCM ni jambo gumu.
Natoka CCM, mimi leo nimeamua kutoka CCM na kujiunga na upinzani wa UKAWA. Uamuzi huu si rahisi watu wetu kuuelewa, nitajaribu kuueleza ili mnielewe, sitoki kwa sababu nina hasira, kukatwa, Simpendi mgombea wake Magufuli bali nakiimarisha chama cha mapinduzi. Mimi ni mwanachama tu na sina nafasi yoyote hata ujumbe wa tawi sina hivyo CCM hawana sababu ya kusikitika.
Nadhani huko nitakapoenda wataona umuhimu wangu, naamini na CCM wataona umuhimu wangu. Better late than never, kuuondoka kwangu CCM sikidhoofishi bali sasa watakuwa na upinzani mkali. They have to pull up their socks, sijadai shilingi.
Sijaingia huku kwa sababu tu Lowassa anatoka Kaskazini au Mbowe ni wa Kaskazini, nilipiga vita siasa za kaskazini. Kina Mbatia, Dr Slaa na Lipumba wamefanya kazi kubwa, Lowassa ana ujuzi hwa wengine wameenda shule lakini hawajakaa katika serikali, CCM imezubaa wanajifanya watashinda lakini wananchi wanataka mabadiliko, ni lazima sisi ambao tuna uchungu na nchi hii tuwasaidie hawa waweze kuendesha nchi hii. Lowassa peke yake na Mbatia hawataweza, lazima wawepo watu wachache wataoweza kuwasaidia kupiga mbizi kwa haraka.
Tunawaomba watu wengine waliopo CCM waje watusaidie, tukiwaacha wataweza lakini watachukua muda mrefu sana.
Mwisho niwashukuru wote ambao nimeshirikiana nao, naishukuru sana familia yangu. Nimekuwa CCM tangu nina miaka 35, mtu ambae anajua miaka yote niko CCM alafu asubuhi anaamka namwambia nimeamka CCM, namshukuru sana, pia nawashukuru wanangu japo walikubali kwa shingo upande.
Chama gani ndani ya UKAWA nitajua mbele ya safari.
Home »
KITAIFA
,
SIASA
» Hizi Hapa Sababu Kuu Kwanini Sumaye Amekihama Chama Cha CCM na Kuamua Kuingia Ukawa..Je Unajua Amehamia Chama Gani?
Hizi Hapa Sababu Kuu Kwanini Sumaye Amekihama Chama Cha CCM na Kuamua Kuingia Ukawa..Je Unajua Amehamia Chama Gani?
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website