Wabunge nchini Afrika Kusini wamepigana bungeni baada ya spika kuamuru
maafisa wa usalama kuwaondoa kwa lazima wabunge wa upinzani ambao
walimbeza rais Jacob Zuma alipoingia bungeni tayari kulihutubia kikao.
Rais Zuma ambaye ameshindwa katika kesi mbili kuu zinazomhusisha na
ubadhirifu wa mali ya umma na usimamizi mbaya alikuwa amefika bungeni
kwa mara ya kwanza tangu kushindwa mahakamani.
Hata hivyo ujio wake uliwakera sana wabunge wa chama cha upinzani Economic Freedom Fighters (EFF).
Wabunge hao chini ya kiongozi wao Julius Malema walipiga mayowe na
kumtupia matusi bw Zuma jambo lililomlazimu spika wa bunge kuamuru
wabunge hao wa EFF kuondolewa nje.
Ijumaa iliyopita mahakama ya juu ya Afrika Kusini iliamua kuwa rais Zuma
anapaswa kufikishwa kizimbani kufuatia kesi za ufisadi dhidi yake.
Kesi hiyo inahusiana na ufisadi uliotokea katika ununuzi wa silaha zenye thamani ya mabilioni ya dola mwaka wa 1999.
Zuma amekanusha madai yote dhidi yake, Anatarajiwa kukamilisha hatamu yake mwaka wa 2019.
Uamuzi huo wa mahakama ulikuwa msumari wa moto kwa kidonda cha Zuma
ambaye mwezi uliopita alipatikana na hatia ya matumizi mabaya ya
madaraka yake alipokaidi amri yakulipa pesa za umma zilizotumiwa
kukarabati nyumba yake ya Nkandla
Wabunge Warushiana Makonde Afrika Kusini
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website