Mtumishi wa Wizara ya Fedha, Aneth Msuya (30) ambaye ni mdogo wa
Bilionea Erasto Msuya aliyeuawa kwa kupigwa risasi 22 KIA, ameuawa kwa
kuchinjwa nyumbani kwake eneo la Kigamboni jijini Dar Es Salaam.
Mmoja wa ndugu wa familia hiyo, Shujaa Khamis, jana alithibitisha kuuawa kwa Aneth, lakini alikataa kuingia kwa undani.
“Ni kweli wamemchinja usiku wa kuamkia leo (jana) na hapa nipo kwenye
msiba hapa nyumbani (Mererani) kwa baba. Tumeambiwa wamechukua Tv tu,”
alisema.
Hata hivyo, Khamis alikataa kueleza lolote kama wana mashaka na mauaji
hayo zaidi ya kuliomba Jeshi la Polisi nchini, kuchunguza kiini cha
mauaji hayo na kuwasaka waliohusika.
Habari nyingine kutoka Wizara ya Fedha, ziliwakariri baadhi ya watumishi
wakisema wamepata taarifa za msiba huo, lakini hawajapewa taarifa
rasmi.
“Tuna taarifa tunazisikia sikia kuwa ameauawa, lakini jana (juzi)
tulikuwa naye kazini ila leo (jana) ndiyo tunasikia amechinjwa na watu
wasiojulikana. Imetusikitisha sana,” alisema mmoja wa watumishi hao
ambaye hakutaja jina kwa kuwa si msemaji.
Kamanda wa mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Andrew Satta alipofutwa jana
kuthibitisha taarifa za mauaji hayo alisema yuko kwenye kikao
Home »
KITAIFA
» Dada wa Bilionea Erasto Msuya Auawa Kinyama Kwa Kuchinjwa Nyumbani Kwake Dar es Salaam
Dada wa Bilionea Erasto Msuya Auawa Kinyama Kwa Kuchinjwa Nyumbani Kwake Dar es Salaam
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website