“Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje”. Hii ni moja ya kauli ambayo Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa aliziongea Arusha May 30 2015 alipotangaza nia ya Kugombea Urais kupitia CCM.
CCM ilikuwa na Wagombea zaidi ya 40 ambao walitangaza nia na kuchukua fomu za Kugombea Urais 2015 lakini baadae Chama hicho kikampitisha Dk. John Pombe Magufuli kugombea nafasi hiyo, baada ya hapo kukawa na taarifa nyingi sana kuhusu ishu ya Edward Lowassa na UKAWA.
Viongozi wa Umoja wa UKAWA wamekutana Dar leo na mmoja wa Viongozi hao, James Mbatia amesema wamekubaliana kumkaribisha Mbunge Edward Lowassa ndani ya UKAWA na wako tayari kumpa nafasi na kushirikiana nae.
Mbatia ameongeza kuwa Lowassa ni mchapa kazi makini na mfuatiliaji wa karibu wa kiutendaji katika majukumu anayokabidhiwa.
Alipoulizwa kuwa Lowassa atakuwa mgombea Urais Mbatia amesema kila chama kina utaratibu wake hivyo mchakato ukishakamilika atatangazwa mgombea urais wa UKAWA mmoja mwanzoni mwa mwezi agosti.
Alipoulizwa kuwa Lowassa atakuwa mgombea Urais Mbatia amesema kila chama kina utaratibu wake hivyo mchakato ukishakamilika atatangazwa mgombea urais wa UKAWA mmoja mwanzoni mwa mwezi agosti.