Ndege za kijeshi za Kenya zimeshambulia maeneo ya wapiganaji wa kundi la Alshabaab katika taifa jirani la Somalia .
Ndege
hizo zililenga maeneo mawili ya jimbo la Gedo,linalotumiwa na
wapiganaji hao kuvuka na kuingia Kenya, msemaji huyo ameongeza.
Maeneo hayo mawili hutumiwa na wapiganaji hao kupanga mshambulizi nchini Kenya.
Wanajeshi wa AMISOM walitarajiwa kupeleka wanajeshi wao katika eneo hilo la Gedo lakini hadi sasa hawajafanya hivyo.
Hili
ni shambulio la kwanza la Kenya kwa shambulizi la alshabaab ambalo
lilisababisha mauaji ya watu 148 katika chuo kikuu cha Garissa wiki
iliopita.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapa kujibu shambulizi hilo kwa njia mbaya zaidi.