Taarifa zinasema kuwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam umemvua kwa muda Mhadhiwa Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Kitila Mkumbo madaraka ya kuongoza Kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam (DUCE).
Hatua hiyo inatajwa kuchukuliwa baada ya uongozi wa UDSM kupata taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa Dk Kitila Mkumbo alikuwa kiongozi wa chama cha siasa, CHADEMA wakati angali ni mtumishi wa umma, jambo ambalo Uongozi wa chuo hicho umekariri kuwa ni kinyume cha sheria ya nchi na Serikali kwa mfanyakazi wa umma kushika wadhifa katika chama cha siasa.
Kutokana na uamuzi wa chuo hicho, Dk Kitila aliandikiwa na kukabidhiwa barua ya kusimamishwa kwake wadhifa huo.
Dk Kitila bado ataendelea kuwa Mhadhiri Mwandamizi kwenye kitivo hicho.