Home » , » BAADA YA WABUNGE KUMUANDAMA,, MH. MIZENGO PINDA AMUAKUFUNGUKA ASEMA ''UWAZIRI MKUU NI MZIGO MKUBWA''

BAADA YA WABUNGE KUMUANDAMA,, MH. MIZENGO PINDA AMUAKUFUNGUKA ASEMA ''UWAZIRI MKUU NI MZIGO MKUBWA''

Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameliambia Bunge muda mfupi uliopita  kwamba kama ikitokea Rais akamng'oa katika nafasi yake ya uwaziri mkuu, yeye  atafurahi sana  kwa kuwa kazi anayoifanya ni mzigo mkubwa.
 
"Kama ningeambiwa LEO ningeondolewa katika nafasi hii, basi dada Rukia mimi ningefurahi kwa kuwa ningekuwa nimetua mzigo.
"Dada Rukia, hii kazi huombi, Rais anaangalia na anakuchagua kuwa Waziri Mkuu. Anaweza kuangalia akakuchagua hata  wewe dada Rukia, kwa hiyo LEO Rais  akisema basi, nianchie ngazi, mimi niko tayari, nitafurahi," amesema Pinda katika kipindi cha maswali na majibu bungeni.
 
Waziri Pinda ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge Rukia aliyetaka  kujua  msimamo wake kutokana na kauli ya Kamati ambayo yeye na mawaziri wengine waliambiwa wapime kama wanastahili kuendelea kuwa mawaziri  kutokana na ufisadi wa kutisha  TAMISEMI.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
 
Copyright © 2011. PERUZI HABARI - All Rights Reserved
Proudly powered by Peruzitz