Home » , , » RAISI MSTAAFU WA BOTSWANA Mh. FESTUS GONTEBANYE MOGAE ALIPOMTEMBELEA RAFIKI YAKE Mh. MOHAMMED DEWJI

RAISI MSTAAFU WA BOTSWANA Mh. FESTUS GONTEBANYE MOGAE ALIPOMTEMBELEA RAFIKI YAKE Mh. MOHAMMED DEWJI

DSC_1899

Mwenyekiti wa MeTL Group Bw. Gulam Dewji ambaye ni baba mzazi wa Mohammed Dewji kwenye mazungumzo na Rais mstaafu wa Botswana Mh. Festus Gontebanye Mogae alipomtembelea rafiki yake Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji (katikati) ofisini kwake.

Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group Mh. Mohammed Dewji siku ya jana alipata nafasi ya kuzungumza na rafiki yake, Rais mstaafu wa Botswana (1998 - 2008) Mh. Festus Gontebanye Mogae. Mh. Mogae aliekua mshindi wa tuzo ya Mafanikio katika Uongozi itolewayo na mfanyabiashara mzawa wa Sudan Bwana Mo Ibrahim mwaka 2008, alikuwa na mazungumzo binafsi na Mohammed Dewji (Mo) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar-es-salaam.
 
 
Tuzo hiyo ya Mo Ibrahim, humuwezesha mshindi kupata kitita cha dola za Kimarekani millioni 5, na dola za Kimarekani 200,000 kila mwaka kwa maisha yake yote. Hizi ni baadhi ya picha, zilizopigwa na mpiga picha wetu, jana kwenye ofisi za MeTL Dar-es-salaam.


president (1)

Mh. Mohammed Dewji katika picha ya pamoja na rafiki yake, Rais mstaafu wa Botswana (1998-2008) Mh. Festus Gontebanye Mogae
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
 
Copyright © 2011. PERUZI HABARI - All Rights Reserved
Proudly powered by Peruzitz