Home » , » Zitto: Tozo ya Tsh 1000 kwa kadi ya Simu yako kila Mwezi imeanza Rasmi..ni Aibu

Zitto: Tozo ya Tsh 1000 kwa kadi ya Simu yako kila Mwezi imeanza Rasmi..ni Aibu

Kodi ya tshs 1000 kwa mwezi Kwa kila kadi ya simu uliyonayo imeanza rasmi.

Bunge la wananchi, wawakilishi wa wananchi, limepitisha kodi hii. Hailipwi na kampuni ya simu, inalipwa na Wewe mwenye simu. Kampuni ya simu inakusanya Kwa niaba ya serikali. Ingawa sikuwepo wakati kodi hii inapitishwa na Bunge siwezi kukwepa wajibu wa kuaibika kuwa sehemu ya Bunge hili.

Ni aibu Kwa kuwa pendekezo la kodi hii liliondolewa na Waziri wa Fedha kwenye hotuba yake ya makadirio ya mapato ya Serikali. Pendekezo lilirudishwa namna gani kupitia muswada wa fedha, finance bill, Haieleweki. Ni skandali. Nasikia vibaya sana kuwa mbunge kwenye Bunge lenye maamuzi ya namna hii. Nasikia aibu zaidi kwamba hatukupiga kelele za kutosha kuzuia jambo hili.
Ameandika Zitto Kabwe.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
 
Copyright © 2011. PERUZI HABARI - All Rights Reserved
Proudly powered by Peruzitz