Qandeel Baloch, aliyekuwa miongoni mwa mastaa wa mitandao ya kijamii
nchini Pakistan, ameuawa na kaka yake katika mji wa Multan uliopo kwenye
jimbo la Punjab. Alidai amemuua dada yake kwa heshima.
Polisi wamedai kuwa Baloch aliuawa na kaka yake kwenye nyumba ya familia
yao baada ya kuchukizwa kwa muda mrefu na picha ambazo dada yake
alikuwa akizipost mtandaoni.
Mwili wa mrembo huyo ukipelekwa kuzikwa
Baada ya kutekeleza mauaji hayo kaka yake alikimbia japo baadaye
alikamatwa na polisi na kukiri kuhusika mbele ya waandishi wa habari.
Msichana huyo alikuwa akiweka picha za kawaida ambazo mastaa wengine duniani hupenda kuziweka kuonesha urembo wao.
Hata hivyo kwa maisha ya Pakistan na sheria zake, Baloch alionekana kuwa ‘controversial’ japo alipendwa sana.
Alikuwa na karibu wafuasi 750,000 kwenye mtandao wa Facebook ambako
video zake zilikuwa maarufu na kuzalisha mijadala nchini humo.
Alijipatia umaarufu zaidi nchini humo baada ya kuahidi kuwa angevua nguo
online kama timu ya Pakistan ingeshinda kwenye mchezo wa cricket dhidi
ya mahasimu wao India.
Baloch alitengeneza pia vichwa vya habari baada ya kupost selfie kwenye
Instagram akiwa na Mufti Abdul Qavi, moja ya viongozi wa dini nchini
humo na kupelekea kusimamishwa wadhifa huo.
Kaka yake alidai kuwa skendo zake ndizo zilimfanya achukue uamuzi wa kumuua.
Bongo5
Home »
BURUDANI
,
UDAKU
» Staa wa Pakistan Auawa na Kaka yake Aliyechukia Picha Alizokuwa Akiweka Kwenye Mitandao ya Kijamii
Staa wa Pakistan Auawa na Kaka yake Aliyechukia Picha Alizokuwa Akiweka Kwenye Mitandao ya Kijamii
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website