Takwimu zilizotolewa na wizara ya afya, maendeleo ya jamii jinsia ,
watoto na wazee nchini zinaonyesha kuwa mkoa wa Dar es salaam na Dodoma
inaongoza kwa vitendo vya mapenzi ya jinsia moja
Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam waziri wa
wizara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu alisema kutokana na hali hiyo wizara
imepiga marufuku matumizi ya vilainishi vinavyotumiwa na baadhi ya
makundi yanayo jihusisha na vitendo hivyo.
Mhe. Ummy Mwalimu alisisitiza kuwa serikali imeamua kuzuia vilainishi
hivyo kwani vimetajwa kuchochea vitendo hivyo ambavyo nikinyume na
sheria na taratibu za nchi nakuongeza kuwa vitendo hivyo nimiongoni mwa
sababu inayochangia ongezeko la VVU.
Aidha Mhe. Ummy alisema kuwa kwa sasa serikali inajikita kuhakikisha
kuwa inajenga wodi za wazai, kununua vifaa tiba, madawa ya kutosha
katika hosptali zake na sio ununuzi wa vilainishi hivyo
Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma Yaongoza Kwa Mapenzi ya Jinsia Moja
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website