Akizungumza
na Amani Kajala alisema kitendo cha kuokoka kimegeuka kama kejeli kwa
marafiki zake ambapo wengi humcheka lakini anaamini kabisa siyo akili
zao bali shetani anataka kuwatumia ili aanguke.
“Kuna
ambao wananicheka kicheko kikubwa kabisa baada ya kusikia kuwa nimeamua
kumfuata Yesu na wengine kunikejeli lakini mimi sina neno naamini
kabisa ni nguvu ya shetani ili nirudi nilikotoka, nawaambia tu watakuwa
wamechelewa sana,” alisema Kajala