Abdu Kiba amesema kuwa promotion ndiyo inawabeba wasanii wa lebo ya WCB.
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM, “Sijafikiria
kuimba na msanii kutoka WCB, kwa sababu sijaona anayeimba type ya muziki
wangu.”
“Hata kama wana promote kwa sababu ndiyo walipoona wao ndiyo wanaweza
wakafanya na watu wakaweza kuelewa lakini siku zote ajuae hazami,”
alisema Abdu Kiba.
Aidha aliongeza kuwa bado hajaona msanii anayeimba type ya muziki wake ndani ya lebo hiyo [WCB].
Hata hivyo mapema mwezi huu msanii huyo alikiambia kipindi cha Planet
Bongo cha EA Radio kuwa yupo tayari kujiunga na lebo ya WCB kama
watakubaliana na kuweka hela mezani kauli ambayo baadaye yeye mwenyewe
aliipinga kuwa watu hawakumuelewa vizuri alichomaanisha.
Abdu Kiba adai wasanii wa WCB wanabebwa na Promo
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website