Hii ni kama filamu lakini ndio ukweli, Diwani wa Kata ya Kiborlon
Manispaa ya Moshi, Frank Kagoma (Chadema) ameonyesha ujasiri wa hali ya
juu alipopambana na majambazi waliokuwa na silaha za moto.
Alinusurika kuuawa baada ya majambazi hao waliokuwa na bunduki na
bastola, kumfyatulia risasi sita alipokuwa akiwafukuza ambazo hata
hivyo, hazikumpata.
Tukio hilo ambalo lilionekana kama sinema, lilitokea mwishoni mwa wiki
iliyopita baada ya majambazi hayo kuvamia duka la jumla la kuuza mitumba
linalomilikiwa na Menti Mbowe na kupora Sh10 milioni.
Katika tukio hilo lililotokea saa tano asubuhi eneo la Kiborlon,
majambazi hayo walimjeruhi kichwani mfanyabiashara huyo anayemiliki pia
mabasi ya Machame Safaris. Hali ya majeruhi huyo inaendelea vizuri.
Diwani Moshi Akwepa Risasi Sita, Apambana na Majambazi Mwanzo Mwisho....
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website