Julai
16, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema kikao
cha Bavicha hakitofanyika kwa sababu itakuwa ni mwendelezo wa vurugu
zao.
Mkutano
Mkuu wa CCM, utakuwa na ajenda mbalimbali ikiwamo ya Mwenyekiti wa
chama hicho, Jakaya Kikwete kumkabidhi kijiti cha uongozi Rais John
Magufuli.
Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius Mwita jana alisema
baraza hilo lipo kwenye hatua ya mwisho ya maandalizi ya kikao hicho
kitakachohudhuriwa na zaidi ya wajumbe 50 kutoka mikoa yote.
“Wajumbe wataanza kuwasili kesho (leo) mjini Dodoma. Hatuna wasiwasi na kikao hiki kwa sababu ni cha ndani siyo mkutano wa hadhara, ambao umepigwa marufuku na polisi,” alisema Mwita.
“Wajumbe wataanza kuwasili kesho (leo) mjini Dodoma. Hatuna wasiwasi na kikao hiki kwa sababu ni cha ndani siyo mkutano wa hadhara, ambao umepigwa marufuku na polisi,” alisema Mwita.
Mwita
alisema kikao hicho kitakuwa cha siku mbili kuanzia Julai 20 hadi 21 na
kwamba, kitahudhuriwa na mameya na wenyeviti vijana wa halmshauri
zinazoongozwa na Chadema.
Alipotafutwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob ambaye ni mwanachama wa Bavicha kujua kama atahudhuria kikao hicho alijibu: “Nitakwenda kwa sababu mimi ni kijana, sina sababu ya kukataa wito wa viongozi wangu wa juu wa Bavicha taifa.”
Kuhusu kauli ya Kamanda Mambosasa, Mwita alisema polisi ilishatoa maelekezo ya kuruhusu vikao vya ndani.
“Taarifa
ya Mambosasa hatujaishangaa kwa sababu ni desturi yake kujichanganya,
leo anasema hivi kesho vile. Tunamtaka atulie asubiri tumpe taarifa ni
wapi kikao chetu kitanyika kwa njia ya amani,” alisema Mwita