Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Balozi Ombeni Sefue amesema baada ya miaka
mingi ya utumishi wa umma sasa ni wakati wake wa kupumzika na hafikirii
kujitosa katika siasa.
Balozi Sefue ambaye alikuwa kivutio kwenye televisheni kutokana na kutoa
taarifa za kutenguliwa uteuzi kwa watumishi waandamizi wa umma kabla ya
kibao kumgeukia, amesisitiza kuwa siasa haipo katika damu na kwamba
kazi anayopenda ni kuzisaidia taasisi za ujenzi kwa kuwa ni taaluma
anayoipenda.
Mbali na kuonyesha kutokuwa na mpango huo, Balozi Sefue aliupongeza
utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa maelezo kuwa una kasi
nzuri na kwamba kurejea kwa uadilifu ni jambo linalomfurahisha zaidi
akiwataka vijana kufanya kazi kwa bidii baada ya kuaminiwa na kupewa
nafasi mbalimbali.
Balozi Sefue ambaye awali hakuonekana kuwa mmoja wa watu ambao
wangeng’olewa kwa sababu yoyote ile, alilazimika kuondoka Ikulu ndani ya
siku 123 tangu Rais Magufuli aapishwe kuwa Rais na siku 67 tangu balozi
huyo atangazwe kuendelea na wadhifa wake. Uteuzi wake ulitenguliwa
Machi 6 na nafasi yake kuchukuliwa na Balozi John Kijazi.
Baada ya kimya cha muda mrefu, Mei mwaka huu, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
(Utumishi wa Utawala Bora), Dk Laurean Ndumbaro alikaririwa akisema kuwa
baadhi makatibu wakuu walioachwa katika uteuzi na Rais, wapo
waliostaafu kwa mujibu wa sheria, akiwamo Balozi Sefue.
Balozi Sefue afunguka..Adai Wakati wake Umefika Sasa
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website