Washukiwa wa kundi la Al-Shabaab mapema leo Alhamisi wameshambulia na
kulipua mtambo wa mawasiliano ulioko katika mji wa Fino, Lafey katika
kaunti ndogo ya Mandera nchini Kenya.
Afisa mkuu wa Polisi huko Lafey, Bosita Omukolongolo, amesema kuwa kisa hicho kilitokea saa nane usiku.
Afisa huyo wa Polisi anasema kuwa walikabiliana vikali na wanamgambo
hao, lakini hakuna maafa yaliyoripotiwa upande wa polisi waliokuwa
wakiulinda mlingoti huo wenye vifaa vya kupeperusha mawasiliano.
Kundi la Al- Shaabab, ambalo lina makao yake nchini Somalia, limehusika
na mashambulizi ya mara kwa mara pamoja na mauaji nchini Kenya na
mataifa kadhaa ya Afrika Mashariki na upembe wa Afrika
Al-Shabab Washambulia Mtambo wa Mawasiliano Kenya
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website