Watu watatu wamejeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari wa vikosi vya
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na kupelekwa hospitali ya Alrahma
kwa matibabu.
Majeruhi hao ni Yussuf Ali Juma (23), Ali Shaame Ibrahim (18) na Salim
Masoud Bakar (18), wakazi wa Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja.
Kabla ya watu hao kujeruhiwa, milio ya risasi ilitawala jana majira ya
saa 8:30 mchana katika mitaa ya Tomondo, Mwanakwerekwe na Kilimani,
hivyo kuzua taharuki miongoni wakazi wa mitaa hiyo.
Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa waliyaona magari ya vikosi hivyo
yakiendeshwa kwa mwendo kasi kuzunguka maeneo hayo huku yakiwa na askari
wakifyatua risasi.
“Mimi kwa sasa nipo hapa Kilimani na hivi punde tu risasi tumezisikia
kutokea upande huu wa Mwanakwerekwe na Jang’ombe na ghafla naona watu
wanakimbizwa kuletwa hapa Alrahma” alisema Rashid Said (54), mkazi wa
Migombani ambaye ni dereva teksi.
Majeruhi Ibrahim alisema: “Walikuja wale mazombi, wengine walifunika uso
waliwafungua ng’ombe wetu na kutaka kuwachukua, kwanza wakapiga risasi
juu, tulipoona wanawapakiza katika magari lao tukasogea ndipo wakatupiga
risasi.”
Bakari Juma (35), mkazi wa Msheleshelini alisema: “Tunasikia hawa jamaa
wanataka wauze kitoweo cha nyama siku za sikukuu peke yao, lakini miye
nasema sawa wafanye hivyo, ila si kwa ng’ombe wa kupora.”
Baadhi ya wananchi walidai kuwa mifugo hiyo wakiwamo ng’ombe wa maziwa ni mali yao.
Mmoja wa wafugaji hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Omar alisema:
“Sisi tunafuga ng’ombe hawa kama mnavyoyaona mabanda yetu yapo si miaka
kumi wala ishirini ni tangu zamani wakati huo Tomondo ni pori tupu na
mpaka sasa mifugo yetu haizururi wala haimkeri mtu yeyote.”
Licha ya askari kudaiwa kufika eneo la tukio na katika hospitali
walikolazwa majeruhi hao, hali ya usalama ilionekana kuyumba pale
makundi ya watu yalipohamasika kusogelea maeneo hayo.
Waliofika katika hospitali hiyo ni pamoja na Mkurugenzi wa Habari na
Mahusiano kwa Umma wa Chama cha Wananchi (CUF), Salim Abdalla Bimani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kufuatilia zaidi ili
kubaini chanzo chake.
Hata hivyo, alisema polisi waliingilia kati na kwenda katika maeneo hayo kurejesha hali ya usalama.
“Sijapata kwa ukamilifu kilichotokea, lakini ni kweli hawa vikosi
wanaendesha operesheni ya kukamata ng’ombe wanaozurura mitaani,
wamekwenda huko na kukatokea kukwaruzana baada ya kuwepo vijana ambao
hawataki kuondoa ng’ombe, nimepeleka askari kutuliza hali na sasa hali
imekuwa ya amani”, alisema Kamanda Mkadam.
Risasi Zarindima Zanzibar ........ Watu watatu Wajeruhiwa
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website