Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Taasisi ya
Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) wamebaini kuwepo na baadhi ya
Makampuni na watu binafsi ambao wamekuwa wakijihusisha na ukwepaji Kodi
ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Kodi ya Mapato kwa kutumia Mashine za
Kielektroniki (EFDs) ambazo hazijasajiliwa na TRA na kutoa risiti
bandia.
Makampuni hayo yamekuwa yakinunua risiti za manunuzi bandia kutoka kwa
watu wanaomiliki mashine za kielektroniki (EFDs) ambazo hazijasajiliwa
na kuzitumia risiti hizo kudai marejesho ya VAT bila kuwepo na bidhaa au
huduma halisi iliyouzwa au kutolewa na muhusika, kitendo ambacho
kinainyima Serikali mapato stahiki kwa mujibu wa sheria.
TRA kwa kushirikiana na TAKUKURU inaendelea na uchunguzi ili kubaini
makampuni yote yanayojihusisha na udanganyifu huu, ambapo hadi sasa
jumla ya makampuni manne (4) yamebainika kujihusisha na ukwepaji kodi
kwa mtindo huu kuanzia mwaka 2010 hadi 2014; na jumla ya shilingi
29,216,900,301.7 imebainika kutokulipwa Serikalini na makampuni hayo kwa
kipindi hicho.
Makampuni hayo manne ni pamoja na Skol Building Material Ltd ambayo
tangu mwaka 2012 hadi 2013 haikulipa jumla ya VAT ya shilingi
5,464,915,963 na Kodi ya Mapato yenye thamani ya shilingi 10,960,787,861
ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni shilingi 16,425,703,824 kwa kipindi
hicho.
Kampuni nyingine ni Farm Plant (T) Limited, tangu mwaka 2010 hadi 2014
haikulipa jumla ya VAT ya shilingi 5,930,170,573 na Kodi ya Mapato yenye
thamani ya shilingi 4,948,393,516 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni
shilingi 10,878,564,089.
Kwa upande wa A.M. Steel & Iron Mills Limited kuanzia mwaka 2013
hadi 2014 haikulipa jumla ya VAT ya shilingi 79,016,112 na Kodi ya
Mapato yenye thamani ya shilingi 131,693,518 ambayo jumla ya kodi
inayodaiwa ni shilingi 210,709,630.
Kampuni nyingine ni A.M. Trailer Manufacturers Limited ambayo tangu
mwaka 2013 hadi 2014 haikulipa jumla ya VAT ya shilingi 638,221,034.80
na Kodi ya Mapato yenye thamani ya shilingi 1,063,701,724.00 ambayo
jumla ya kodi inayodaiwa ni shilingi 1,701,922,758.80
Baada ya kubaini ukwepaji kodi wa makampuni hayo, TRA kwa kushirikiana
na TAKUKURU inaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizi na mara baada ya
uchunguzi kukamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya
watakaobainika kukwepa kodi.
“Ni wito wangu kwa wafanyabiashara wote kutojihusisha na kununua risiti
za bandia na kudai marejesho ya (VAT) yasiyostahili kwakuwa Mamlaka
imejidhatiti kuendelea na zoezi hili la kuwabaini wafanyabiashara wanao
kwepa kodi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kwa hatua stahiki”.
Alisema Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata.
Imetolewa na:
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa pamoja.
Home »
KITAIFA
,
SIASA
» Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika
Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website