MKUU wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanha Jerry Muro ameitwa
kwenye kikao cha kamati ya maadili cha Shirikisho la Mpira wa Miguu
Nchini TFF kufuatia kitendo chake cha kupingana na kuishambulia katika
kuelekea mechi yao ya Kimataifa ya kombe la Shirikisho Barani Afrika
uliofanyika Juni 28.
Hiyo inakuwa ni mara ya tatu kwa Muro kuitwa na anatakiwa kufika Julai
02 katika ofisi za TFF saa Nne asubuhi au kama atashindwa kufika basi
atume mwakilishi wake au utetezi wake kwa njia ya maandishi.
Muro amethibitisha hilo na kusema kuwa amepokea barua hiyo na hii ikiwa
ni mara ya tatu na katika mara zote amekuwa anashinda kwa hoja na
kwa.wakati huu mkakati wao mkubwa kuona nafungiwa kujihusisha na masuala
ya mpira na zaidi anashangaa ni jinsi gani wanasema amewashambulia
kupitia vyombo vya habari.
Barua hiyo inamtaka Muro kujitokeza siku hiyo au hata kama hatoweza
kufika basi atume utetezi wake kwa maandishi au mwakilishi wake na hata
kama hatofika basi kikao cha kamati ya maadili kitaendelea kama kawaida
na watatoa maamuzi kama kawaida.
Jerry Muro Aitwa Kamati ya Maadili TFF....Kisa Hichi Hapa
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website