Msanii Baraka da Prince amekanusha vikali kumshika msanii wa kike wa
bongo fleva sehemu za kifuani, na kusema aliyepiga picha hiyo aliikuza.
Akiongea kwenye eNews ya East Africa TV, Baraka amesema hajwahi kufanya
kitendo kama hicho kwani walikuwa sehemu yenye watu wengi, na pia
hajawahi kuwaza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Linah.
“Siwezi kufanya kitu kama hicho kwa sababu pale pana watu wengi, ile
picha ilikuwa ya kawaida, yule aliyeipiga na kuipost amekuwa kama
kaikuza, sijawahi kufikiria hata kutoka naye”, alisema Baraka.
Pia Baraka amesema siku ya tukio ambayo ilikuwa ni siku ya kuadhimisha
miaka 10 ya muziki wa Christian Bella, aliondoka mapema na hakufanya
tukio lolote baya.
“Nimetoka kuperfom nikaondoka zangu, sikukaa hata nusu saa, nimemaliza
nikaondoka, wasiwe wanaamini mambo ya hivyo”, alisema Baraka
Home »
BURUDANI
,
UDAKU
» Baraka da Prince Afunguka Kuhusu Yeye na Linah Baada ya Picha ya Utata Kuzagaa Mtandaoni
Baraka da Prince Afunguka Kuhusu Yeye na Linah Baada ya Picha ya Utata Kuzagaa Mtandaoni
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website