sitaki kumuudhi wala kumkera kwa lolote, namtimizia kila kitu ili mradi tu asipate vishawishi vya kutoka nje ya ndoa!
toka tuanze mahusiano yetu ya kindoa, mke wangu alikuwa msikivu sana kwangu, kila ninalo mwambia amekuwa
akinisikiliza! ilifikia kipindi ikawa ni utamaduni wetu kuwa tuna share mpaka simu zetu! yeye akiwa anatumia yangu mi
natumia yake! wiki chache hivi zilizopita, nimeshangazwa sana na hiki kitendo nilichokuta kwenye simu ya mke wangu, simu yake imefungwa kwa namba maalum anazozijua yeye mwenyewe!! nilipojaribu kuhoji juu ya hilo, akanijibu kwa ukali, ''kwani wewe unataka nini, simu si yangu, na wewe una yako.. funga na wewe yako''!
niliamua kukaa kimya ili nisizue mengine! mke wangu amekuwa ni mtu wa kupokea simu za ajabu ajabu na kutumiwa meseji kila mara, kila ninapohoji, yeye anasema kwa ukali kwamba wivu, namwaibisha kwa mashoga zake... eti tuko mjini hapa!!!
mwenzenu nimechanganyikiwa!!! nahisi kunyang'anywa tunda langu''.....