Home » » MERTESACKER, OZIL NUSURA WAZICHAPE KUFUATIA KIPIGO CHA 6-3

MERTESACKER, OZIL NUSURA WAZICHAPE KUFUATIA KIPIGO CHA 6-3

Pointing the finger: Per Mertesacker (right) explodes at Mesut Ozil following Arsenal's 6-3 defeat against Manchester City
Akimnyooshea kidole, acha mambo yako mwana!:  Per Mertesacker (kulia) akimuwakia  Mesut Ozil baada ya kula kipigo cha mabao  6-3 kutoka kwa Manchester City

KIPIGO siku zote kinavuruga!!. Baada ya Arsenal kuburuzwa kwa kipigo cha mabao 6-3 kutoka kwa Manchester City, Wachezaji wawili wa klabu hiyo raia wa Ujerumani, Per Mertesacker na Mesut Ozil wamepigana mkwara mzito wakati wakitoka nje ya uwanja wa Etihad.
Mertesacker alimuwakia vikali Ozil ambaye ni rafiki mkubwa katika soka na kumnyooshea kidole kiungo huyo baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa.
Hali hiyo imetokea baada ta Ozil kushindwa kuwapungia mkono wa heshima mashabiki wa Gunners waliosafiri ugenini.
Wakati wawili hao wakizozana, kocha mkuu wa klabu hiyo, Arsene Wenger alicheka tu na kusema: “Waache Wajurumani, watamalizana wenyewe, msijali”.
Mabao ya City yamefungwa na Sergio Aguero dakika ya 14, Alvaro Negredo dakika ya 39 Fernandinho mawili dakika za 50 na 88 David Silva dakika ya 66 na Yaya Toure dakika ya 90.
Theo Walcott alirejea uwanjani kwa mara ya kwanza leo tangu Septemba na kufanikiwa kutundika nyavuni  mabao mawili ya Arsenal dakika za 31 na 63, wakati lingine lilifungwa na beki Per Mertesacker dakika ya 90.
Boiling over: Mertesacker continues to rage against his close palAcha hizo!: Mertesacker akiendelea kumuwakia rafiki yake mkubwa katika soka
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
 
Copyright © 2011. PERUZI HABARI - All Rights Reserved
Proudly powered by Peruzitz