UBUYU uliokolea rangi jijini ni kwamba staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford
anadaiwa kuchumbiwa na mfanyabiashara maarufu Bongo, Chid Mapenzi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo karibu na mwanaume huyo kilieleza
kuwa, wawili hao wapo kwenye mipango lukuki ya kufunga pingu za maisha
na mwanzoni mwa wiki hii Chid alifunga safari hadi ukweni mkoani Dodoma
kutoa mahari ambayo haikufahamika ni kiasi gani cha fedha.
Baada ya kuunasa ubuyu huo, shushushu wetu alitafuta ‘kontakti’ za
msanii huyo aliyewahi kujizolea umaarufu na Filamu ya Chausiku,
alipoulizwa alionesha mshktuko na kuangua kicheko;
“Khaa! Huo ubuyu kiboko, hakuna kitu kama hicho jamani, mimi yule ni
mtu wangu wa karibu tu isitoshe kwetu siyo Dodoma, watu bwana!”
Mwigizaji Shamsa Ford Adaiwa Kuchumbiwa
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website