Home » , » Mr Blue adai couple anayoikubali zaidi ni ya Diamond na Zari

Mr Blue adai couple anayoikubali zaidi ni ya Diamond na Zari


        Rapper Mr Blue amesema Diamond na Zari ndiyo couple anayoikubali zaidi.

“Ukinitoa mimi na Wahyda couple ambayo naipenda, naielewa ni Zari na Diamond,” Blue alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM.

“Yaani wanapendeza unajua eeh, na Mungu amewajaalia wamepata mtoto, wanashirikiana kama marafiki kwenye biashara, wanajua kucheza na akili za raia, wanaitengeneza couple yao ya kimapenzi, wanaifanya pia inakuwa kibiashara, yaani very nice,” aliongeza.

Kwa upande mwingine Blue amesema hana kabisa bifu na Diamond.

“Sina bifu na Diamond na juzi tumekutana naye Mwanza kwenye show ya Ne-Yo alivyokuja, tumeongea vizuri, tumesalimiana, safi kabisa.”
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
 
Copyright © 2011. PERUZI HABARI - All Rights Reserved
Proudly powered by Peruzitz