Waziri mkuu wa Uingereza, David
Cameron, ametangaza atajiuzulu, baada ya kushindwa kuwashawishi raia
wengi wa Uingereza, kusalia katika muungano wa Ulaya.
Bw Cameron ambaye ameongoza kampeini ya kusalia katika muungano wa EU amesema kauli hiyo imempa mshutuko mkubwa na kwa baadhi ya watu mashuhuri duniani.