Bajeti
ya Serikali iliyotangazwa huenda ikapunguza idadi ya watu wanaopenda
kuonekana tofauti, kwenye usajili wa magari kwa kuandika majina yao
badala ya namba.
Wamiliki
wa magari wanaotaka kusajili namba binafsi kama kuweka majina yao, sasa
watalipa Sh10 milioni badala Sh5 milioni za awali, kwa kipindi cha
miaka mitatu.
Akitoa
mapendekezo ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2016/17 jana,
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango aliomba Bunge liridhie
kufanya marekebisho ya Sheria ya Magari (Kodi na uhamisho wa umiliki)
ili kupandisha usajili wa namba hizo.