Uking’atwa na nyoka ukiguswa na jani lazima utaruka.
Baada ya kuvunjika kwa mahusiano na Nuh Mziwanda, taarifa za chini
zimezidi kuenea kuwa Shilole ana mahusiano ya kimapenzi na msanii
chipukizi wa Bongo Fleva, Nerd aliye chini ya label ya Ommy Dimpoz, PKP.
Akiongea kwenye kipindi cha Busati, kinachoruka kupitia Magic FM, Shilole amesema hana mpenzi kwa sasa.
“Mimi mpenzi wangu ni hela, Nerd ni rafiki yangu. Ukiwa kwenye mapenzi
unakuwa kama kipofu unakuwa hauoni. Ukimkabidhi mtu moyo wako anakuwa
anaufinyanga, kwa sasa moyo wangu umestawi tofauti na zamani,”
aliongeza.
Hata hivyo Shilole amesema hana namba ya Nuh Mziwanda na hajawahi
kuwasiliana naye tangu walipoachana. Kwa sasa muimbaji huyo ana wimbo
mpya uitwao Say My Name
Mwambaji Shilole Ataja Mpenzi Wake wa Sasa...
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website