Taarifa ya uteuzi huo imetolewa na Katibu Mkuu (Uchukuzi), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leornald Chamurinho ambapo imeeleza kuwa uteuzi huo unaanza Februari 22 mwaka huu.
Kabla ya uteuzi huo, Johari alikuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Walaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA – Consumer Consultative Council).
Mkurugenzi Mkuu huyo mteule amejaza nafasi iliyokuwa ikikaimiwa na Redemptus Bugomola