Mume wangu ana tatizo la kuwahi kumwaga. Yaani dakika 2 tu ameshamaliza na kuniacha nikiwa nateseka huku nikiwa nina hamu. Tatizo hili limekuwa linanisababishia maumivu ya tumbo na kiukweli nikiwa naye sikuwahi kufika kileleni na kwa kuwa alinioa nikiwa bikira sikuweza kugundua mapema tatizo ni la nani.
Muda mwingi nilikuwa najichukia na kuwaza huenda mimi ndio nina tatizo na yeye mwenyewe wakati nikilalamika alikuwa ananiambia kuwa mimi ndio nina tatizo kwanini kila siku sifiki kileleni; mara nilikuwa siko tayari basi tu ilimradi nionekane tatizo liko kwangu.
Basi siku moja niliamua kujaribu nje, lol sitasahau ilikuwa ndio siku yangu ya kwanza kujua raha ya mapenzi. Sasa toka wakati huo nimekuwa simpendi kabisa mume wangu na nina mpango niachane naye kwani mbali na kutokuwa mzuri kitandani pia hatoi huduma kwa familia, kiufupi ni mvivu kila idara.
Naombeni ushauri wenu nifanyeje ili niweze kuachana naye coz siwezi kuishi na mume ambaye anamaliza haja zake tu (mbinafsi)