Akiongea jana kwenye hafla iliyoandaliwa na wasanii kumuaga Rais Jakaya Kikwete, Diamond alidai kuwa hayo ni sehemu ya maendeleo kwenye muziki yaliyotokea katika mihula miwili ya uongozi wake.
“Katika miaka hii 10 na mtoto nimepata. Mheshimiwa mtoto amezaliwa leo (jana) lakini amepata endorsement leo leo karibuni milioni 50 katika duka tu la kuwa anadhaminiwa kama mtoto anavalishwa na hilo duka, sio maendeleo hayo jamani,?” alihoji Platnumz.
Diamond hakusita pia kuzungumzia rekodi ilivyovunjwa na akaunti ya Instagram ya mwanae, ambayo hadi sasa ina followers zaidi ya elfu 45 siku moja tu baada ya kuzaliwa.
“Katika Afrika ndio mtoto wa kwanza huyo aliyepata followers wengi Afrika nzima, anatokea Tanzania sio maendeleo hayo?